Hayo yamesemwa leo tarehe 29 Aprili, 2025 na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Geita Manispaa Ndg. Yefred Myenzi wakati akifungua mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili kwa waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki yaliyofanyika katika Ukumbi wa Gedeco.
Myenzi amesisitiza watendaji kuwa makini katika mafunzo haya pia kuwa waadilifu na kuhakikisha hawajihusishi na itikadi ya chama chochote wakati wa zoezi la uboreshaji na uandikishaji wa awamu ya pili
Pia amewasisitiza watendaji hao kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na tume na kuyafanyia kazi lakini pia kulinda viapo vyao vya kutunza siri kwa maana kutoa taarifa kwa asiyehusika ni kosa kisheria na kunaweza kukupelekea kuhukumiwa kufungwa jera kuanzia miaka 20
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndg. Ray Lema amesema kuwa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili utafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 07 Julai, 2025.
Ameongeza kuwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata ambapo jumla ya vituo 23 vitahusika,
Ndg. Ray amesema zoezi hili litahusisha kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi ambao hawakujiandikisha kwenye zoezi la kwanza na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk ametembelea mafunzo hayo na amewaasa watendaji hao kuwa makini ili waweze kuifanya kazi yao kwa weledi.
Karibuni mtazame namna Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Ndg. Yefred Myenzi akihamasisha jamii kukata leseni za biashara na kufuatilia zoezi la ukusanyaji mapato kwa jumla
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa