Halmashauri ya Mji kupitia Idara ya Kilimo imekuwa ikisimamia na kutoa ushauri kwa wakulima juu ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na elimu ya ushirika kwa wanachama wa AMCOs, SACCOS na vyama vya ushirika vya msingi.
Kulingana na ardhi na hali ya hewa katika Halmashauri ya Mji wa Geita baadhi ya mazao kama Katani, dengu, tumbaku na alizeti yanaweza kustawi vizuri yakilimwa katika maeneo mbalimbali lakini wakulima hawajapata mwamko wa kuyalima isipokuwa alizeti tu ambayo inalimwa kwa kiwango kidogo sana na wakulima wachache.
Kusoma maelezo mafupi juu ya Sekta ya kilimo bofya maandishi ya bluu hapo chini
MAELEZO YA HALI YA KILIMO GTC.pdf
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa