UTANGULIZI
Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini ni moja ya Divisheni nyeti na muhimu sana katika Halmashauri ya Mji ya Geita kutokana na kushughulika na miundo mbinu ambayo ni uhitaji mkubwa kwa maisha ya kila siku si tu kwa Wakazi wa Halmashauri ya Mji Geita bali kwa Tanzania kwa ujumla.
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA
• Kufanya ukaguzi wa barabara na madaraja
• Kutayarisha bajeti ya mwaka ya matengenezo ya barabara na madaraja
• Kusimamia kazi za barabara na madaraja zinazotekelezwa na makandarasi
• Kufanya ukaguzi wa majengo ya halmashauri yanayojengwa kwa kutumia mafundi na wakandarasi
• Kusimamia kazi za majengo zinazotekelezwa na makandarasi
• Kutoa ushauri na kusimamia ujenzi wa majengo ya serikali katika ngazi ya kata na vijiji. Miradi iliyosimamiwa ni Ujenzi wa ofisi za Kata, vyumba vya madarasa, maabara, zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya.
Pia Idara ya Ujenzi inasimamia Mitambo mitatu ambayo ni Greda, Excaveta na Rolla,Mitambo hii inatumika kukarabati barabara za Halmashauri ya Mji na pia ukodishwa kwa wakandarasi watakaokuwa na kazi ndani ya Halmashauri ya Mji.
HALI YA WATUMISHI KATIKA IDARA
Idara ina idadi ya watumishi kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini:
Kada/Nafasi
|
Waliopo
|
Mkuu wa Idara
|
1
|
Mhandisi wa Majengo
|
1
|
Mhandisi wa Barabara
|
1
|
Msanifu Majengo
|
1
|
Mafundi Sanifu Ujenzi
|
4
|
Jumla |
8 |
UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA IDARA
Idara ya Ujenzi ilianza kupokea fedha za matengenezo ya barabara kutoka Mfuko wa Barabara (Road Fund) mwaka wa fedha 2013/2014. Kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Idara iliidhinishiwa bajeti kiasi cha Tshs. 1,046,400,000/= kwa ajili ya matengenezo ya barabara,Mfuko wa Barabara (Road Fund) umekuwa ukiidhinisha bajeti inayoombwa na Idara kwa ajili ya Matengenezo ya Barabara kila Mwaka wa fedha.
MRADI WA UBORESHAJI MIJI
Halmashauri ya Mji Geita ni miongoni mwa miji 18 ya Tanzania Bara inayotekeleza mradi wa Uboreshaji Miji (Urban Local Government Strengthening Program) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Miji mingine ni Tabora, Morogoro,Shinyanga, Sumbawanga, Moshi, Musoma, Songea, Singida, Iringa, Kibaha, Babati, Korogwe, Mpanda, Lindi, Njombe, Bukoba na Bariadi.
Kupitia mradi huu tumefanya usanifu wa barabara za Mji Km. 18 zitakazojengwa kwa kiwango cha Lami kati ya sasa na 2018.
Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 tulitumia Kiasi cha Tshs. 2,300,000,000/= kujenga barabara ya Jimboni (Km. 2.2) kwa kiwango cha lami ikiwa ni pamoja na kuweka taa za barabarani na njia ya waenda kwa miguu. Mradi huu uliongeza mtandao wa barabara za lami kufika Km. 6.9,Mwaka wa fedha 2016/2017 tunatarajia kujenga barabara ya Miti Mirefu 1 (Km. 0.7) na Miti Mirefu 2 (Km. 0.7) pamoja na Americanchips – Katundu (Km 1.2) ambazo zikikamilika tutakuwa na mtandao wa barabara za lami zenye urefu wa Km.9.5.
MRADI WA UBORESHAJI WA MIJI BARABARA YA JIMBONI (KM 2.2) KABLA AIJATENGENEZWA
MRADI WA UBORESHAJI WA MIJI BARABARA YA JIMBONI (KM 2.2) WAKATI WA UTENGENEZWAJI
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa