SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA YA KILIMO
Kutoa mafunzo ya kanuni bora za kilimo kwa wakulima ikiwemo upandaji kwa nafasi na kwa wakati, matumizi ya pembejeo, zana na teknolojia za kisasa, teknolojia za umwagiliaji na kilimo hai. Mafunzo haya yanatolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo mihadhara, mijadala, mashamba darasa na mashamba ya mfano.
Kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo ya kilimo kwa kupanga na kugawa matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji kwa eneo.
Kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo, mfano ni wapi pembejeo zinapatikana, hali ya masoko, uwezesho wa kifedha na hata mashirika yanayowasaidia wakulima kupata mahitaji yao mbalimbali
Kuwasaidia wakulima kuanzisha na kutunza vitalu vya mbegu za mboga na matunda kwa ajili ya kukuza mazao ya bustani
Kufanya maonesho mbalimbali kupitia siku za wakulima, na hata ngazi ya wilaya kupitia maonesho ya nanenane.
Kutoa mafunzo ya hifadhi ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika na matumizi ya viuatilifu vya mazao ya kilimo ghalani.
Kuwatembelea wakulima, kuona changamoto wanazokutana nazo na kutoa ushauri wa jinsi ya kutatua changamoto hizo.
Kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wakulima ili kuwahamasisha wenzao kupenda kufanya vizuri zaidi. Hii inaleta ushindani ambao hatimaye unasababisha ongezeko la uzalishaji kwa ujumla
Eneo linalofaa kwa kilimo katika Halmashauri ya Mji wa Geita lina ukubwa wa Hekta 51,600 ambapo kwa wastani eneo linalolimwa ni Hekta 31,200
Ukubwa wa eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni Hekta 11,250 na kilimo cha umwagiliaji ( Rain feed) ni Hekta 6200
Eneo linalolimwa kwa wastani wa kaya ni Hekta 2 hadi 5
Hali ya joto ni nyuzijoto 25 hadi 30
Hali ya upatikanaji wa mvua ni kuanzia milimita 700 hadi 1200
Mvua za vuli huanza mwezi Septemba hadi Januari na mvua za kipindi cha masika huanza mwezi Februari hadi Mei kila mwaka.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa