Halmashauri ya Mji wa Geita ina vivutio vinavyoonyesha maeneo ya kale yaliyokuwa yakitumika na ambayo yanaendelea kutumika kwa ajili ya matambiko mbalimbali kama Bao la kale lililoko kwenye mwamba, unyayo wa mtu wa kale ulioko kwenye mwamba, kisima cha maji kisichokauka kilichoko juu ya mwamba, jiwe lililoko juu ya mwamba lenye umbo la ramani ya Afrika na jiwe linaloonyesha umbo la ng'ombe aliyelala. Vivutio vyote vilivyoelezewa hapo viko katika kata ya Bulela. Katika mji wa Geita kuna majengo ya kale, kiwanja na chanzo cha maji kisichokauka kama kivutio kwa ajili ya kumbukumbu kwa wakazi wa Geita mjini.
Uwepo wa Mgodi mkubwa wa Dhahabu wa Geita kwenye mitaa ya Nyamalembo na Nyakabale katika kata ya Mtakuja. Ni mgodi wa pili kwa ukubwa Afrika kwa uzalishaji wa dhahabu. Picha hapo chini ikionesha machimbo ya ndani( underground pit) katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita ambayo ni kivutio kikubwa kwa wageni watokao nje ya nchi na watanzania wenyewe kwa ujumla.
Picha hapo juu ikionesha Uchimbaji wa Madini ndani ya miamba( underground Pit) katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita
jiwe-lenye-ramani-ya-ngombe-aliyelala-linapatikana-katika-kata-ya-bulela
Chemchemi ya Lwenge katika kata ya Kalangalala ambayo haikauki tangu enzi za ukoloni. Inahudumia sehemu kubwa ya wakazi wa Geita mjini kwa maji safi na salama na inasemekana kuna nyoka mkubwa katika eneo hilo ambaye anatokea mara kadhaa akitokea kwenye chanzo cha maji kilipo alimaarufu Keita Abantu( Mlimani).
Moja ya choo kilichokuwa kinatumiwa na wahunzi wakati wa enzi za utawala wa Mjerumani. Choo hicho kipo katika Mtaa wa Lwenge Geita mjini
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa