Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ndg. Mohamed Gombati, mapema leo ametembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo, jijini Mwanza, ambapo ameeleza kufurahishwa na maandalizi mazuri na ushiriki wa halmashauri kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo na Mikoa mingine
Miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea ni banda la Halmashauri ya Manispaa ya Geita, ambapo alipata nafasi ya kujionea ubunifu, huduma na elimu mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi kuhusu kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa.
Ndg. Gombati aliipongeza Manispaa kwa maandalizi mazuri na namna walivyojipanga kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo. Pia, aliwapongeza wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ( Kikundi cha vijana cha Safina Group) kwa matumizi sahihi ya mikopo hiyo.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa