Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Myenzi, ametembelea banda la Halmashauri ya Manispaa ya Geita katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza, ambapo amejionea kwa karibu namna shughuli mbalimbali za maonesho zinavyotekelezwa.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Myenzi alielezea kuridhishwa kwake na maandalizi yaliyofanywa na Idara ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, akiwapongeza kwa jinsi Wanavyo toa elimu kwa wananchi, kuonesha teknolojia bunifu, na kuhamasisha matumizi ya mbinu bora za kilimo na ufugaji.
Baada ya kukamilisha ziara yake katika banda la Manispaa, Mkurugenzi Myenzi aliendelea kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ambapo pia alishuhudia shughuli mbalimbali za maonesho na kutoa pongezi kwa ushiriki wao madhubuti unaolenga kuelimisha wakulima na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa