Idara ya Afya katika Halmashauri ya Mji wa Geita imepanga kutekeleza majukumu yafuatayo ili kuboresha huduma za afya kwa jamii
Mapambano dhidi ya Malaria
Idara ya Afya inaendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria. Idara imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali kama vile kupima wagonjwa wote wenye dalili ya malaria na homa ( joto kali la mwili) kwa kutumia kipimo cha haraka cha malaria na hadubini, kutoa tiba sahihi ya malaria kwa wagonjwa waliogundulika kuwa na ugonjwa huo, ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu kwa akinamama wajawazito (waliohudhuria kliniki kwa hudhurio la kwanza na watoto wa umri chini ya mwaka mmoja waliohudhuria kliniki kwa ajili ya kupata chanjo ya surua.
Pia elimu ya afya ya kujikinga na mbu waenezao ugonjwa wa Malaria inaendelea kutolewa, kadhalika wananchi wanahimizwa kuhusu umuhimu wa kupima kwa kipimo cha haraka cha malaria kwa wagonjwa wote wenye homa, kuwapatia tiba sahihi na matumizi ya vyandarua vyenye viuatilifu kwa kugawa vipeperushi na mabango katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya. Pia shughuli za uelimishaji jamii kuhusu ugonjwa wa malaria zinaendelea kufanywa na wahudumu wa Afya wa jamii( community Change Agents, CCA) katika kila kata kwa kutoa elimu ya kujikinga na malaria kwa kufanya mikutano ya hadhara, kutembelea kaya na kutoa elimu katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa