Kamati hii inaundwa na Wenyeviti wa Kamati zote za Kudumu na Wajumbe wengine na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja. Aidha madaraka na nafasi ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingine za Kudumu na hivyo kisheria haina uwezo wa kufanya kazi za Kamati nyingine za Kudumu. Kwa ujumla majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kupitia vikao vyake.
Majukumu maalumu ya Kamati
(a) Kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti na Mpango wa Maendeleo ili kupata idhini ya Halmashauri.
(b) Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni na kuomba vibali maalumu kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
(c) Kufikiria na pale inapowezekana kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu Sheria Ndogo na utendaji katika ngazi za chini ya Halmashauri.
(d) Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri.
(e) Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri
(f) Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauria mikopo yote yaHalmashauri.
(g) Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa kifungu 18 cha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290.
(h) Kupokea na kujadili taarifa za Wakaguzi wa Fedha na mali za Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa kifungu 54 cha Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 290
(i) Kutoa mapendekezo ya aina ya bima za kuchukuliwa na Halmashauri kwa ajili ya mali zake mbalimbali kwa mujibu wa Kanuni za Fedha (local Government Financial Memorandum), 1997 vifungu 310 – 315.
(j) Kusimamia na kudhibiti masuala yote ya mapato na matumizi ya Halmashauri kwa mujibu wa Kanuni na taratibu za fedha kama inavyelekezwa kwenye Kanuni za Fedha (Local Government Financial Memoranda) ya 1997 kifungu Na. 3 (a).
(k) Kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali zinavyotozwa na Halmashauri, kama inavyoelekezwa kwenye Local Government Financial Memorandum),1997 Na. 3 (c)
(l) Kupokea na kuamua juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni.
(m) Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na miji mingine duniani.
(n) Kusimamia makusanyo na matumizi ya vijiji kwa kifungu 51 (3) cha Sheria ya Fedha ya Sheria za Mitaa (Sura 290)
(o) Kuteua Wakaguzi wa Fedha/mali za Serikali za Vijiji, kwa mujibu wa kifungu 51 (3) cha Sheria ya Fedha za Seriakali za Mitaa (Sura ya 290)
(p) Kuangalia na kupendekeza masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri
(q) Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu mafunzo ya watumishi
(r) Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba, usafiri, matibabu na kupendekeza masuala yanayohusu gharama za mazishi.
(s) Kupitisha mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi.
(t) Kushughulikia maafa katika eneo la Halmashauri.
(u) Kupendekeza kwa Halmashauri kutunga Sheria Ndogo zinazohusu Kamati hii.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa