Wachezaji 43 wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita walioteuliwa kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA mwaka huu, wamepewa hamasa maalum kabla ya kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mashindano hayo ya kitaifa.
Katika tukio hilo maalum la kuwaaga wachezaji, viongozi mbalimbali wa manispaa wamewatakia kila la heri na kuwahimiza kushiriki kwa bidii, wakitambua kuwa wanawakilisha nembo ya Manispaa ya Geita pamoja na Mkoa kwa ujumla.
Akizungumza na wachezaji hao, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Bi. Ellah Makese aliwapongeza kwa kuchaguliwa kushiriki mashindano hayo, akisisitiza kuwa ana imani kubwa na uwezo wao. “Michezo ni afya, lakini pia ni heshima kwa taasisi. Nendeni mkaonyeshe uwezo wenu, mkipata ushindi katika kila mchezo ikiwezekana,” alisema.
Bi. Ellah alisisitiza umuhimu wa kurejea na ushindi, kwani kufanya hivyo kutajenga taswira chanya kwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Mkoa mzima wa Geita.
Akihitimisha hotuba yake kwa ari na matumaini, alihamasisha: “Twendeni Tanga, turudi na ushindi!”
Mashindano ya SHIMISEMITA yanatarajiwa kuanza Tarehe 15/08/2025 na kumalizika tarehe 29/08/2025 yanajumuisha watumishi kutoka sekta mbalimbali za serikali, yakilenga kuimarisha afya, mshikamano, na motisha kazini kupitia michezo.
MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa