Halmashauri ya Mji wa Geita inapatikana kati ya mita 1,100 hadi 1,300 toka usawa wa Bahari. Pia inapatikana kati ya Nyuzi 2o8 hadi 3o28 kusini mwa Ikweta na Nyuzi 32o45 hadi 37o mashariki mwa Greenwich. Halmashauri ya Mji Geita inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Wilaya ya Sengerema na Wilaya ya Nyang'hwale na ina eneo la kilometa za mraba 1080.3 Halmashauri ya Mji Geita ilipata hadhi ya kuwa Halmashauri baada ya kufuata taratibu zote za kisheria na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 280 la tarehe 24 Agosti 2012 na Cheti cha usajili kutolewa tarehe 5 Septemba 2012. Sheria iliyotumika kuidhinisha Mamlaka na eneo la Halmashauri ya Mji ni Sheria Namba 8 ya Mwaka 1982. Kabla ya kuwa Halmashauri kamili, ilikuwa ni Mamlaka ya Mji Geita iliyokuwa chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita kufuatia taarifa kwenye Gazeti la Serikali Namba 353 la tarehe 17 Septemba 2004. Makao makuu ya Halmashauri yapo Geita mjini mtaa wa Magogo, barabara kuu itokayo Mwanza kuelekea Bukoba.
Asili ya jina Geita: Neno Geita limetokana na maneno matatu ya kabila la Wayango (Warongo) ambayo ni Akabanga keita abhantu likiwa na maana kupotea kwa mazingara ambayo yalikuwa kwenye mlima huo wa Akabanga keita abhantu uliokuwa ukitumiwa na warongo kama eneo la mitambiko ya jadi.Jina hili la Geita lilikuwa maarufu kutokana na wazungu kushindwa kutamka maneno Akabanga keita abhantu na hivyo kukatisha kuwa Geita hadi leo.Makabila yaliyokuwepo ya Wazinza, Wasukuma,Wasumbwa na Wasubi wakaigiza matamushi ya wazungu Geita na hivyo neno la Akabanga keita abhantu likaanza kupotea polepole hadi leo.
UTAWALA KABLA YA WAKOLONI
Kabla ya kuingia kwa wakoloni (Wajerumani na Waingereza) Geita ilikuwa na tawala za asili saba (7) ambazo ni:
UTAWALA
|
CHIFU/MTEMI
|
MAKAO MAKUU
|
Busambilo
|
Ludomya Ng’hwele
|
Nyarubele
|
Msalala
|
Musa Chasama Mbiti
|
Kitongo
|
Buyombe
|
Mgunga Kadama
|
Busanda
|
Buchosa
|
Paulo Lukakaza
|
Nyakalilo
|
Kharumo
|
Alexander Gerevas
|
Kharumo
|
Bukoli
|
Mganila Nonga
|
Bukoli
|
Mwingiro
|
Nyorobi Mapumba
|
Idetemya Mwingiro
|
Wakoloni wa kwanza kuingia Geita walikuwa ni wajerumani ambao utawala wao ulikuwa ni wa moja kwa moja(Direct rule) na hivyo kushindwa kabisa kwani wawakilishi wao waliokuwa wakiletwa toka makao makuu Bagamoyo(Pwani) walikuwa wakiuwawa na wenyeji.
Utawala wa pili ulikuwa wa waingereza baada ya vita kuu ya pili ya dunia,ambao wao walitumia utawala usikuwa wa moja kwa moja(Indirect rule) yaani kwa kuwatumia machifu/watemi wa maeneo husika ili kutekeleza azma/malengo yao.
Eneo la mji wa Geita aliwekwa Liwali Petro Nyango ambaye alifanya kazi chini ya utawala wa kwa eneo la mjini.
BARAZA LA JADI (NATIVE AUTHORITY)
Baraza hili lilikuwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Wilaya(DC) wa kikoloni,liliundwa na watemi 7 na liwali 1.Mwenyekiti wa baraza hilo alitokana na watemi hao.Aidha katibu wa baraza hilo alitokana na watemi au karani kutoka ofisi ya DC.
Makao makuu ya baraza hilo yalikuwa mjini Geita eneo jirani na Benki ya CRDB, kila mtemi alijengewa nyumba ya kupumnzikia na kulala.
MAJUKUMU YA BARAZA HILO
Historia ya Wahe. Wenyeviti wa Halmashauri ya Mji Geita
JINA LA MWENYEKITI |
MWAKA ALIOCHAGULIWA |
MWAKA ALIOTOKA MADARAKANI |
MARTINE KWILASA |
2012 |
2016 |
LEONARD K.BUGOMOLA |
2016 |
2020 |
COSTANTINE M. MORANDI |
2021 |
ANAENDELEA |
Hali ya Hewa
Eneo la Halmashauri ya Mji lina tabia ya joto la wastani kuanzia Nyuzi 22oC hadi 30oC. Eneo hili hupata Mvua ya wastani wa milimita 1200 kwa mwaka ambazo huanza kunyesha kuanzia Mwezi Oktoba hadi Januari na Kati ya Mwezi Machi na katikati ya Mei. Kiwango cha unyevunyevu ni kati ya 35% na 60% wakati wa kiangazi na masika.
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Halmashauri ya Mji ina jumla ya wakazi 361,671 .Shughuli za kiuchumi katika Halmashauri ya Mji wa Geita ni kilimo, ufugaji, uchimbaji wa madini ya Dhahabu na biashara mbalimbali ndogondogo, za kati na kubwa.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa