Halmashauri ya Mji wa Geita ina Kitengo cha Manunuzi na Ugavi ambacho kimeundwa kwa mujibu wa sheria ya Manunuzi Namba 07 ya Mwaka 2011 Kifungu 37 ambapo sheria hiyo inaitaka Taasisi ya Serikali iwe na Kitengo cha Ugavi (Procurement Management Unit).
Kitengo cha Ugavi kinatakiwa kiwe na Mkuu wa Kitengo mwenye elimu aliyo somea ujuzi huo na sifa, uzoefu katika kazi za manunuzi na pia awe amesajiliwa na Bodi ya manunuzi (Professional Body) kama Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011 kifungu Na 37(3) kinavyoeleza.
Kwa mujibu wa sheria, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi ataripoti moja kwa moja kwa Afisa Masuuli (Mkurugenzi) wa taasisi husika.
Afisa Masuuli wa taasisi atahakikisha kwamba Kitengo cha Manunuzi na Ugavi (PMU) kinatengewa fedha kwenye bajeti ili kiweze kutimiza majukumu yake.
Majukumu ya Kitengo cha Manunuzi na Ugavi yametajwa katika Sheria ya Manunuzi ya Umma namba 7 ya Mwaka 2011 Kifungu cha 38 (a-q).kama ifuatavyo:
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa