MALIASILI
Utangulizi
Ofisi ya Maliasili katika Halmashauri ya Mji Geita inaundwa na Sehemu tatu ambazo ni Misitu, Wanyamapori, na Kitengo cha Ufugaji Nyuki.
i.) WANYAMAPORI
Kutumia Sheria ndogo za hifadhi ya misitu katika kudhibiti uharibifu wa Mazingira. vilevile Kudhibiti uvunaji wa Wanyama na Misitu pasipo kufuata taratibu katika Pori la hifadhi ya wazi la Geita, kwa kufanya doria za mara kwa mara na elimu kutolewa kwa jamii zinazozunguka hifadhi ya Geita juu ya manufaa ya uwepo wa rasilimali hizo.
ii) MISITU
Tunahamasisha wanavijiji vinavyopakana na hifadhi ya Msitu wa Geita kutoshiriki katika shughuli zinazofanya uharibifu wa Misitu na kushiriki kikamilifu kudhibiti Moto ndani ya Msitu wa hifadhi ya Geita.
Halmashauri ya Mji Geita ina jumla ya Misitu ya hifadhi miwili ambayo ni Msitu wa hifadhi ya Geita yenye ukubwa wa hekta 47,700, na Msitu wa hifadhi ya Usindakwe wenye ukubwa wa hekta 450. Misitu hii inasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Lakini pia sambamba na kuhimiza upandaji Miti katika Halmashauri ya Mji Geita. Tunahimiza Watu kuhifadhi Miti ya asili, jambo ambalo limewezesha Watu binafsi na Taasisi kutunza jumla ya hekta 369.1 ya Miti ya asili katika maeneo yao.
ii.) NYUKI
Kuhamasisha kufuga Nyuki kisasa kwa Vikundi vya Ufugaji Nyuki, na kutembelea maeneo ya wafuga Nyuki ili kutoa elimu ya ufugaji Nyuki kisasa kwa vitendo. Halmashauri ina jumla ya Wafugaji wa Nyuki 5 wenye jumla ya Mizinga 450 na vikundi 3 vyenye jumla ya Mizinga 191. Hivyo katika Halmashauri ya Mji Geita ipo jumla ya Mizinga ya kisasa 641 ambayo huzalisha asali kwa wastani wa kilogramu 20 kwa Mzinga.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa