Idara ya Maendeleo ya Jamii ni Idara mtambuka ambayo hutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na idara nyingine na Wadau wa Maendeleo. Shughuli zilianza kutekelezwa na idara kuanzia Novemba 2012.
Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Jamii :-
(i) Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na
taratibu zinazohusiana na maendeleo ya jamii;
(ii) Kuwezesha jamii kuanzisha, kupanga, kutekeleza na kutathmini wao wenyewe programu na miradi;
(iii) Kuandaa mipango na miradi ya muda mfupi na mrefu katika maendeleo ya jamii katika ngazi ya Halmashauri;
(iv) Kufanya utafiti na kupendekeza jinsi ya kushughulikia matatizo mbalimbali ya maendeleo yanayosimamia maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana na maendeleo ya jamii na wadau wengine
(v) Kusimamia uendeshaji wa ngazi ya watoa huduma wa Taasisi Ndogo za Fedha chini ya maelekezo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT);
(vi) Kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya kiuchumi kwa wanawake ,watoto na watu wenye ulemavu
(vii) Kuratibu utoaji wa mafunzo ya kuondoa umaskini, UKIMWI, dawa za kulevya na usawa wa kijinsia;
(viii) Kuratibu na kufuatilia shughuli za NGOs na CBOs katika jamii
(ix) Kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii katika Halmashauri.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa