Kamati hii itashughulikia mambo yote yanayohusu viwanda, biashara, madini, bustani na ukaguzi wa nyama kwa mujibu wa kifungu cha 62 (c & f) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Sura ya 288).
Kadhalika itashughulikia masuala yanayohusiana na ldara ya Afya na Elimu yakiwemo yahusuyo kinga, tiba, malezi bora ya watoto na akina mama, wazazi, elimu ya awali, msingi, sekondari, watu wazima na maendeleo vijijini.
Majukumu maalum ya Kamati
(a) Kupendekeza kwa Halmashauri mipango ya kupanua biashara na jinsi ya kukusanya mapato,
(b) Kuandaa na kupendekeza mipango madhubuti ya maendeleo ya kilimo,
(c) Kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika,
(d) Kubuni mbinu za kutafiti, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii,
(e) Kupendekeza mipango madhubuti ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati,
(f) Kushauri na kupendekeza mipango madhubuti ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa shule za awali na za msingi kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na. 25 ya 1978 kama ilivyorekebishwa mwaka 1995.
(g) Kushauri na kupendekeza mipango ya kuimarisha kuendeleza elimu ya watu wazima kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na. 25 ya 1978 kama ilivyorekebishwa mwaka 1995.
(h) Kupendekeza matumizi ya mila nzuri zinazoliletea Taifa heshima na zinazoleta maendeleo, pamoja na kupendekeza kuondolewa kwa mila zinazoliaibisha Taifa,
(i) Kupendekeza mipango ya ujenzi au upanuzi wa viwanja, majengo na mazingira ya burudani, starehe, mapumziko na michezo,
(j) Kupendekeza mambo yanayohusu uhifadhi wa mambo ya kale na mandhari mbalimbali yenye sura nzuri
(k) Kupendekeza na kuratibu njia bora ya uhifadhi wa nyaraka muhimu kwa ajili ya kumbukumbu za historia pamoja na uanzishaji wa maktaba za Halmashauri ambazo kumbukumbu hizo zitahifadhiwa,
(l) Kupendekeza njia bora za uhifadhi wa sanaa mbalimbali za ufundi na za maonyesho,
(m) Kupendekeza matumizi mazuri ya lugha ya Taifa
(n) Kupendekeza matumizi ya malezi ya vijana ili waweze kuwa wazalishaji katika Taifa,
(o) Kupendekeza kwa Halmashauri kutunga Sheria Ndogo zinazohusu Kamati hii,
(p) Kuhakikisha kuwa Sera za Uchangiaji katika Elimu na Afya zinatekelezwa,
(q) Kupendekeza kwa Halmashauri kushughulikia magonjwa ya mlipuko.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa