Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari( TEHAMA)
Kutayarisha mpango Mkakati wa kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kuishauri Menejimenti ya halmashauri ya masuala yanayohusiana na sera zinazohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
Kuishauri Menejimenti ya halmashauri juu ya masuala yanayohusiana na sera, miongozo na taratibu zinazohusiana na takwimu.
Kusimamia maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wake kwa ajili ya halmashauri.
Kutoa na kuratibu msaada wa teknolojia ya habari kwa menejimenti ya halmashauri.
Kutathimini, kuboresha na kusimamia teknolojia ya habari na mawasiliano na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye halmashauri.
Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo
Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na namna ya kuthibiti.