Katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Duniani 2025, elimu juu ya umuhimu wa kunyonyesha watoto maziwa ya mama imetolewa kwa wazazi katika Zahanati ya Geita Town na Kituo cha Afya Nyankumbu.
Afisa Lishe wa Manispaa ya Geita, kwa kushirikiana na watoa huduma wengine wa afya, wameendesha mafunzo kwa vitendo kwa kina mama kuhusu mbinu bora za unyonyeshaji.
Mambo ambayo wazazi wamejifunza ni pamoja na:
1. Umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekeendani ya miezi sita ya mwanzo na kuendelea hadi mtoto atakapofikisha miaka miwili.
2. Namna sahihi ya kunyonyesha (kupitia maonesho ya vitendo/demo).
3. Changamoto zinazokwamisha unyonyeshaji na mbinu za kukabiliana nazo.
4. Kuondoa dhana potofu kuwa maziwa ya mama ni machafu.
Elimu hii imelenga kuhamasisha afya bora kwa watoto wachanga na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika kupitia lishe bora tangu hatua za awali za maisha.
#WikiYaUnyonyeshaji2025
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa