Halmashauri ya Mji wa Geita ina jumla ya shule za msingi 93, shule 65 zikiwa ni shule za Serikali na shule 28 zikiwa ni za watu binafsi. Jumla ya wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza hadi la saba ni 90,000, wavulana 45,293 na wasichana 46,747.
Utekelezaji wa Elimu Msingi bila malipo
Katika kutekeleza azma ya Serikali ya kutoa elimu msingi bila malipo, Halmashauri ya Mji imeendelea kusimamia utekelezaji wa Waraka wa Elimu Namba 3 wa mwaka 2016 unaotoa mwongozo wa namna ya kutekeleza elimu ya msingi bila malipo. Waraka wa Elimu na 3 umeweka bayana majukumu ya wadau wote muhimu katika utoaji wa elimu msingi bila malipo ambapo imeainishwa kuwa wazazi /walezi wanantakiwa kufanya yafuatayo
i. Kununua sare za shule na michezo, vifaa vya kujifunzia, chakula kwa wanafunzi wa kutwa na kugharamia matibabu kwa watoto wao.
ii. Kulipia nauli ya kwenda shule na kurudi kwa wanafunzi wa kutwa
iii. Kulipa nauli za wanafunzi wakati wa likizo, kununua vifaa kwa ajili ya malazi shuleni na vifaa vya kujifunzia
Halmashauri ya Mji Geita imeendelea kuhamasisha jamii / wananchi ili wajitolee nguvu kazi na mali kwa lengo la kuleta maendeleo ya shule zilizo katika maeneo yao. Ikumbukwe kwamba waraka wa Elimu Na. 3 hauzuii wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na elimu bali umezuia michango iliyokuwa inawalenga moja kwa moja wanafunzi, wazazi au walezi. Michango ya namna hiyo ilikuwa inasababisha wanafunzi kufukuzwa shule / kurejeshwa nyumbani na kukosa masomo iwapo mzazi au mlezi angeshindwa kuilipa michango hiyo mapema. Pia wazazi wajenge utamaduni wa kukagua kazi za shuleni za watoto wao ili kujiridhisha kama wanafundishwa shuleni.
Elimu Sekondari
Halmashauri ya Mji wa Geita ina jumla ya shule 34 za Sekondari, kati ya hizo shule 24 zinamilikiwa na Serikali na shule 10 zinamilikiwa na watu binafsi pamoja na mashirika ya dini. Shule za Serikali zina wanafunzi 12,005 ambapo wavulana ni 6,143 na wasichana ni 5,862.
Halmashauri ya Mji kupitia Idara ya Elimu Sekondari imeweza kufanya shughuli zifuatazo;-
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa