Maabara ya Kwanza ya Ujenzi Yajengwa Geita Mjini
Kukamilika kwa ujenzi wa Maabara inayojengwa katika makao makuu ya Halmashauri ya Mji wa Geita kwa ajili ya kupima vifaa vya ujenzi wa barabara( materials) kama vile mchanga, udongo, kokoto, mawe nk kutawezesha urahisi wa kufanikisha vipimo vyote vya muhimu vinavyotakiwa kufanywa kabla ya kuanza kazi za ujenzi wa barabara.
Akizungungumza na mwandishi wa habari hii, Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijjini na Mijini( TARURA) Geita Mji , Mhandisi Theresa Bernado amesema kuwa hatua za ujenzi wa maabara hiyo ni wa kuridhisha na baada ya usajili wake kukamilika kulingana na taratibu zilizowekwa itafunguliwa rasmi kwa ajili ya kuanza kazi.
Mhandisi T. Bernado ameongeza kuwa baada ya usajili kukamilika maabara itaajiri watumishi ambao watakuwa na uwezo wa kuhudumia kazi zote za ujenzi wa barabara ndani nan je ya Halmashauri ya Mji wa Geita kwa ufanisi na umakini wa hali ya juu.
Kwa upande wake Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Mhandisi Ipyana Mwamwembe ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi huo amesema shughuli ya ujenzi wa maabara hiyo utakapokamilika kwa asilimia 100 watakabidhi jengo hilo kwa TARURA ambao ndio wataratibu shughuli zote za upimaji wa vifaa vya barabara. Maabara hiyo imejengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 70 kutoka fedha za mpango wa uboreshaji miji( ULGSP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa