Wananchi wa Manispaa ya Geita wamejitokeza kushiriki zaoezi la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita ikiwa ni Jumamosi ya Mwisho wa mwezi huku Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Ndugu. Yefred Myenzi akiongoza zoezi hilo leo tarehe 28 Juni, 2025 katika Kata ya Kalangalala
Shughuli hii ya Usafi ni muendezo wa kampeni Ya HYAGULAGA GEITA (SAFISHA GEITA) iliyo zinduliwa na Mhe Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba Tarehe 26 Aprili, 2025 ikiamasisha watu kufanya usafi na kuisafisha Geita kuwa safi na yenye kupendeza
Mkurugenzi wa manispaa ya Geita Ndugu. Myenzi ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kufanya usafi kila wakati katika maeneo yao na siyo kungoja siku ya Jumamosi pekee ameyasema hayo huku akisisitiza wananchi kuendana na hadhi ya manispaa kwa kuisafisha Geita
Naye Mtendaji wa Mtaa wa Nyerere Road Ndg. George Mabuga amesema kuwa anawapongeza wananchi na wafanya biashara waliojitokeza na kuunga mkono zaezi la usafi pia ameahidi kuendelea kuunga mkono kampeni ya hii ya safisha Geita kwa kuendelea kuweka mabango ya kuhamasisha usafi.
Huku Wananchi waliojitokeza wamesema wanaendelea kuunga mkono na kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa na Mkuu wa Wilaya kwa kampeni hii inayohimiza usafi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa