Halmashauri ya Manispaa ya Geita inaendelea na maandalizi ya mashindano ya SHIMISEMITA
Hayo yamebainishwa siku ya Jumamosi tarehe 28 Juni, 2025 na Bi. Mary Nehemiah, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, wakati wa Bonaza la watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba lililofanyika katika viwanja vya Shule ya wasichana Nyankumbu iliyopo katika Manispaa ya Geita.
Bi. Mary amesema, pamoja na kuwa michezo inajenga afya na kuimarisha urafiki, Manispaa inaendelea kujipima kimichezo ili kuhakikisha inafanya vyema katika mashindano ya SHIMISEMITA na kuhakikisha inarudi na makombe ya kutosha kama ishara ya ushindi
Katika bonaza hilo Halmashauri ya Manispaa ya Geita iliibuka mshindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Halmashauri ya Kwimba katika mchezo wa mpira wa miguu kwa wanaume.
Wakati Halmashauri ya Kwimba iliibuka kidedea katika mchezo wa mpira wa mikono (netball) kwa wanawake kwa goli 15 kwa 14 dhidi ya Manispaa ya Geita
Nao watumishi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya kwimba wameishukuru Manispaa ya Geita kwa Mapokezi mazuri na kuwezesha ufanyikaji wa bonaza hili
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa