Halmashauri ya Manispaa ya Geita kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini leo tarehe 04 Julai, 2025 kimetoa elimu ya Habari na Saikolojia kwa Wanafunzi wa kozi ya awali ya Jeshi la Akiba yanayoendelea katika Kata ya Kalangalala, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwajengea uwezo wa kitaaluma na kisaikolojia ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi katika mazingira mbalimbali ya kijamii na kijeshi.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ndg. Justine Mbilinyi amesema kuwa kwa hali ya sasa, askari anahitaji si tu ujuzi wa kijeshi, bali pia uelewa wa kina kuhusu Elimu ya Habari na kufahamu mienendo ya binadamu kupitia saikolojia ya msingi.
“Vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika jamii yoyote inayolenga maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni hivyo elimu ya habari itawasaidia kuelewa umuhimu wa mawasiliano sahihi, matumizi ya vyombo vya habari, na tahadhari dhidi ya taarifa za upotoshaji” alieleza Mbilinyi
Naye, Mpiga Picha wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndg. Damasen Leonard akiwasilisha mada ya Saikolojia amesema,
"Elimu ya saikolojia inawapa uwezo wa kutambua hali za kiakili na kihisia za watu, hali inayosaidia kujenga uhusiano mzuri baina ya askari na jamii"
Ndg. Damasen ameongezea kusema, Askari wa Jeshi la Akiba ana nafasi kubwa katika kuleta utulivu, usalama na mshikamano wa kitaifa. Ili kutimiza wajibu huo kikamilifu, ni lazima awe na uelewa mzuri wa saikolojia ya watu na pia aweze kutofautisha kati ya jambo sahihi na lisilo sahihi katika utekelezaji wa majukumu yake. Nidhamu, weledi, uadilifu na huruma ni nguzo za mafanikio kwa askari yeyote anayetaka kulitumikia taifa kwa heshima.
Akizungumza kwa niaba ya Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Geita na wanafunzi, MT 82691 Drill SGT wa kozi Simon Lazaro Byejwe katika Wilaya ya Geita ambaye ni Msaidizi wa Mshauri wa Jeshi la akiba wamekishukuru Kitengo cha Mawasiliano kwa Elimu waliyoitoa na kufurahishwa na masomo hayo, akisema kuwa limewasaidia kujitambua, kujenga uwezo wa mawasiliano bora, na kupata maarifa yatakayowasaidia ndani na nje ya jeshi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa