Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Ndg. Mohamed Gombati amewakumbusha watumishi wa umma kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano pasipo kusahau kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita katika kikao kilichofanyika leo tarehe 30 June, 2025 kwenye Ukumbi wa mikutano wa EPZA.
Ndg. Mohamed Gombati amewasisitiza watumishi kutambua kuwa kila mmoja kulingana na kada yake ni mtu wa muhimu katika kuhakikisha shughuli za Serikali zinafanywa kikamilifu na kwa kuheshimiana pasipo kusahau viapo vyao vya kazi na utunzaji wa siri za ofisi kwa lengo la kuongeza umakini wa kazi pamoja na kuzisaidia Halmashauri kutimiza vyema majukumu yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenzi amemshukuru Katibu Tawala wa Mkoa kwa kuitisha kikao kazi hiki ambacho pia kiliwezesha watumishi kutoa changamoto na ushauri ambao utasaidia kuchochea maendeleo ya Manispaa na Mkoa wa Geita kwa ujumla
Naye Afisa Habari wa Mkoa wa Geita, Bi. Trovina Kikoto amekipongeza Kitengo cha Habari kwa namna ya kinavyojulisha Umma juu ya matukio mbalimbali yanayoendelea katika Manispaa na kukitaka Kitengo kuhakikisha kinafikia na miradi ya maendeleo
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa