Watumishi Wa Umma Wakumbushwa Kuwa Waadilifu
Watumishi wa Umma katika Wilaya ya Geita wamekumbushwa kuwachukulia wananchi ambao ndio wateja wao kama wafalme kwa kuwahudumia kwa upendo na uadilifu pasipo kusahau kutumia kauli nzuri na lugha yenye staha wakati wa mazungumzo baina yao.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita Ndugu. Thomas Dimme wakati alipokuwa akifungua rasmi Maadhimisho ya Juma la Watumishi wa Umma tarehe 19/6/2020 katika Halmashauri ya Mji wa Geita, Maadhimisho ambayo yaafanywa kwa kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara na Vitengo vya Halmashauri katika mabanda kwenye viwanja vya Gedeco.
“Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita amesema kuwa watumishi wa Umma wana wajibu wa kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia bidi ya kazi, uadilifu, weledi, kujituma na kutoa huduma bila upendeleo. Maonyesho yamewezesha Halmashauri kupata mrejesho kutoka kwa wananchi ambao wanafika kwenye mabanda ya Idara kuwasilisha shida zao zinazohitaji utatuzi.” Aliongeza Thomas Dimme.
Ndg. Thomas Dimme ameongeza kuwa Watumishi wa Umma watumie juma hilo kujitathimini endapo huduma wanazozitoa zinaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya tano. Pia ameziagiza mamlaka zote zilizoko katika Wilaya ya Geita kuboresha mifumo ya utatuzi wa kero na malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa na wananchi kwa kuwa na sanduku la maoni na daftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu ya malalamiko yote yanayowasilishwa katika ofisi zao.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Mji Geita Bi. Thecla Gasembe amesema kuwa wiki ya Utumishi wa Umma huadhimishwa kwa malengo mbalimbali ikiwemo kupata mrejesho kutoka kwa wananchi na wadau wanaohudumiwa ili kurekebisha kasoro za utendaji dhidi ya Taasisi ya Umma zitakazobainishwa. Pia ni kutambua mchango na umuhimu wa Watumishi wa Umma katika kuleta maendeleo katika Taifa lao.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Halmashauri ya Mji Geita yameanza tarehe 16/6/2020 na yatahitimishwa tarehe 23/06/2020. Kauli mbiu iliyotolewa na Umoja wa Afrika ni “Jukumu la Utumishi wa Umma katika Kujenga na Kudumisha Amani iliyopo Miongoni mwa Jamii”.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa