• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

BILIONI 19.1 KUTEKELEZA UJENZI KITUO KIKUU CHA MABASI MANISPAA YA GEITA

Posted on: June 6th, 2025

Hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Kituo cha Mabasi imefanyika leo tarehe 06 Juni, 2025 katika Ukumbi wa EPZA uliopo Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita Mkoani Geita. Mgeni rasmi katika hafla hii alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba.

Mhe. Komba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji Saini wa Mkataba huo, amemtaka mkandarasi anaetekeleza mradi huo kuhakikisha anazingatia muda wa mkataba kwa kuwa kituo kinachotumika kwa sasa hakikidhi matarajio.

“Na tumeanza safari pamoja ya kuhakikisha mkandarasi anatimiza malengo ambayo ya Mkataba, mradi huu uanze  kwa wakati na ukamilike kwa wakati” Amesema Mhe. Komba

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe. Costantine  Kanyasu  amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa wa stendi  hii ya mbasi.

Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Costantine Morandi amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuwa wavulivu kwa kipindi kirefu wakisubiria stendi hii mpya na ya kisasa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndg. Yefred Myenzi akiwa katika hafla hiyo amesema ujenzi huo utagharimu zaidi ya Bilioni 19 ili kuondoa adha waliyokuwa wakiipata wananchi na watumiaji wote kwa ujumla katika kituo cha sasa hususani kipindi cha mvua.

“Tumefurahi kwa sababu sasa serikali imetoa pesa Bilioni 19.1 kwa ajili ya ujenzi mpya ya kisasa ambayo kama ambavyo tulivyoshuhudia mkandarasi amesaini na tumeahidiwa kwamba tarehe 15 tayari atakuwa kazini kwa ajili ya kuendelea na taratibu” amesema Myenzi

Mkataba huo umesainiwa baina ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Mkandarasi M/s SIHOTECH Engineering Company Ltd. na AMJ Global Multi Contractors Company Ltd na Gharama ya Mkataba huo ni TZS 19,171,601,509.00 ambapo Muda wa utekelezaji wake ni Miezi 15 kuanzia tarehe 15 Juni, 2025 hadi tarehe 14 Septemba, 2026 na utekelezaji huu unafanyika kupitia mradi wa uboreshaji Miji Tanzania (TACTIC).

Stendi hiyo mpya itajengwa katika kiwanja namba 01, kitalu "G" chenye ukubwa wa mita za mraba 109,450 sawa na hekta 10.9 kilichopo  Mtaa wa Magogo, Kata ya Bombambili. Eneo hili limetengwa mahsusi kwa matumizi ya stendi ya mabasi na linamilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Geita.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram

Facebook

X

Youtube

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA GEITA June 03, 2025
  • TANGAZO KUHUSU FURSA ZA MIKOPO YA ASILIMIA 10 May 27, 2025
  • Zaidi

Habari Mpya

  • BILIONI 19.1 KUTEKELEZA UJENZI KITUO KIKUU CHA MABASI MANISPAA YA GEITA

    June 06, 2025
  • WATUMISHI GEITA MANISPAA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA

    June 05, 2025
  • WATUMISHI WA MANISPAA YA GEITA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MITANDAO YA KIJAMII YENYE TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

    June 04, 2025
  • ZIARA YA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI VITUONI

    June 03, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa