Leo Juni 11, 2025 Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanya Mkutano maalumu wa Baraza wa kujadili majibu ya hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Uwekezaji Cha Manispaa ya Geita uliopo Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita Mkoani Geita ukiongozwa na Mhe. Fatma Mwassa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Mhe. Fatma amewataka Watumishi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma ili kuepuka kuzalisha hoja ambazo zinaweza kuichafua Manispaa.
Aidha, Mhe. Fatuma ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo jambo lililopelekea Halmashauri kuendelea kupata hati safi.
Naye, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Costantine Morandi amemshuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia Manispaa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Ndg. Yefred Myenzi ameishukuru Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa kazi wanayofanya na ameahidi kuwa kutekeleza kwa wakati mapendekezo na ushauri uliotelewa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa