Kamati ya Uratibu wa Mwenge kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Geita, imepitia na kukagua miradi mbalimbali, pamoja na njia iliyopendekezwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili Mkoani Geita mnamo tarehe 1 Septemba, mwaka huu ambapo, Halmashauri ya Manispaa ya Geita, itakua ya pili kuupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Geita tarehe 2 Septemba, 2025.
Akizungumza tarehe 25, Juni wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Deodatus Kayango ameiagiza Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha kuwa maandalizi yanakuwa vizuri pamoja na kuziweka nyaraka zote muhimu za miradi ili Mkoa uweze kufanya vizuri.
Aidha, kamati hiyo pia imetoa mapendekezo kwa timu ya Wahandisi kuhakikisha wanaikagua miradi hiyo mara kwa mara ili kujiridhisha, kuzingatia huduma zote za msingi; Maji na Umeme zinapatikana kwenye miradi hiyo, pamoja na kuwakazania Wakandarasi waweze kuikamilisha miradi hiyo kwa wakati.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa