Mkurugenzi Myenzi ameinisha hayo, wakati alipokuwa akijibu swali la Mkuu wa Wilaya Geita Mhe. Komba alipotembelea Zahanati ya Nyakahengele iliyopo katika Kata ya Ihanamilo ikiwa ni sehemu ya Kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata hiyo.
Akiwa katika Kata ya Ihanamilo, Mhe Komba amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Nyakahengele, mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Igenge, mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati ya Bunegezi na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Mtaa wa Ikulwa.
Katika ziara hiyo, Mhe. Komba aliambatana na Katibu Tawala Wilaya, Kamati ya Usalama Wilaya, Mkurugenzi wa Mji, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Mji, Afisa Tarafa ya Geita na Wakuu wa Taasisi za TANESCO, TARURA na GEUWASA
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa