Hayo yameelezwa Katika Kikao Kazi kati ya Wakuu wa Vitengo na Idara zote mbili za Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Geita Wilaya, kilichofanyika katika Ukumbi wa EPZ eneo la Bombambili leo tarehe 11/07/2025.
Katika Kuwapongeza kwa Jitihada kubwa Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashimu Komba katika Kikao Kazi chake na Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu Yefred Myenzi na Wakuu wa Idara Manispaa ya Geita wakawa wanafanya kikao cha Tathimini kwa Mwaka 2024/2025. Na moja kati ya Hatua kubwa ni kwa Kuvuka lengo la Kukusanya Mapato kwa 2024/2025 kwa kufika 100.23% ya Shilingi Bilioni 19.9 Mkuu wa wilaya aliweka Msisitizo kwenye:-
Mwelekeo Bora na wakuleta Ufanisi kuelekea Mwaka wa Fedha 2025/2026 kwa kuwataka Wakuu wa Idara na vitengo kuweka Michango chanya kwenye Ukusanyaji wa Mapato kwa kutoa Elimu, Ushirikishwaji Zaidi wa Watumishi wote, Kutatua Changamoto za ukusanyaji wa Mapato ya Mwaka wa fedha uliopita, ufuatiliaji, na kubuni mbinu mpya.
Pia Mhe. Komba amewataka Watumishi kuwa na ushirikiano na upendo unaodumisha Amani kuongeza Ufanisi Kazini. Kwa vile matokeo chanya ya Taasisi yanategemea jitihada za mtu mmoja mmoja na wote kwa Ujumla, hivyo tutegemeana na kupeana Ushirikiano.
Ameeleza tamanio lake ni kuona Halmashauri inatoa Huduma Bora kwa Wananchi kama vile Shule, afya na Ustawi wa jamii ya Geita, lakini pia motisha na kuhamasishana Sisi kwa sisi kufika malengo kusudiwa.
Wakizungumza kwa nyakati Tofauti Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Geita , wamesisitiza matumizi Bora ya Vifaa vya TEHAMA na mitandao ya kijamii kuhabarisha umma na kutoa Elimu sahihi kwa Wananchi na sio upotoshaji na kukaa kimya bila ya Kusema yale mambo mema ambayo Serikali inafanya kwa wananchi wake.
Mwisho, Mhe Mkuu wa Wilaya alimalizia kwa kuwasihi Watumishi kujiandaa na Uchaguzi mkuu October 2025, kwa kuwasaidia Wagombea kupunguza Manung’uniko ya Wananchi kwa kutatua kero Zao.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa