Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ametembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Geita Mkoa wa Geita, ambapo ameonesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake.
Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Aweso amesema Mradi huo ni mwarobaini wa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji kwa Wakazi wa Geita
“Nimeridhishwa sana na kasi ya utekelezaji wa Mradi huu ndugu zangu wana Geita wali wa kushiba huonekana kwenye sahani, Mradi huu unaenda kuzalisha lita milioni 45 mara mbili ya mahitaji ya sasa ya lita milioni 22 Mradi huu ni matumaini mapya kwa Wananchi wa Geita” Mhe. Aweso.
Aidha katika ziara hiyo Aweso amempongeza Mkurugenzi wa GEUWASA Mhandisi. Frank Changawa kwa kazi kubwa ya usimamizi wa utekelezaji wa mradi huo na bidii ya kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela, alitumia nafasi hiyo kumshukuru Waziri kwa kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mradi huo, akibainisha kuwa ni mradi wa kimkakati unaoleta unafuu mkubwa kwa wakazi wa Manispaa ya Geita.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, ameipongrza Serikali kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku akisisitiza ushirikiano wa karibu wa Serikali na wananchi katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa ufanisi na kutoa matokeo chanya kwa jamii.
Mradi wa Maji wa Miji 28 Geita mpaka sasa umefikia Asilimia 68 za utekelezaji na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2025.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa