MKURUGENZI WA MANISPAA YA GEITA AKIAMBATANA NA MAAFISA ELIMU MSINGI AKABIDHI GARI AINA YA COSTA KWA UONGOZI WA SHULE YA MSINGI BOMBAMBILI.
Idara ya elimu Msingi kwa kushirikiana na uongozi wa shule ya Msingi Bombambili pamoja na wazazi imenunua gari aina ya Costa toka kampuni ya MRC Investment Tanzania LTD.
Mapema leo tarehe 23 Juni 2025 Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Ndugu Kapela Kahamba amekabidhi nyaraka za gari hiyo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita ili aweze kuikabidhi kwa uongozi wa shule
Baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Ndugu Yefred Myenzi Kukabidhi Gari hiyo amesema gari hiyo imenunuliwa Kwa kupitia michango mbalimbali ya wazazi shuleni hapo kwa lengo mahususi la kupunguza changamoto za usafiri kwa wanafunzi katika Shule hiyo .
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa