Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amewataka watumishi wote katika mkoa wa Geita kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 01 Mei, 2025 wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala
Mhe. Shigela amesema kuwa hakuna mtumishi ambaye ana umri chini ya miaka kumi na nane hivyo wote wenye sifa waende kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga ambapo utawapa kibali cha kuchagua viongozi ambao watakuwa chachu katika kujali na kuthamini haki na maslahi ya wafanyakazi.
Kwa mkoa wa Geita Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili unafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura na umeanza leo tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 07 Julai, 2025.
Aidha, Mhe. Shigela amewapongeza viongozi wa vyama wa wafanyakazi mkoani Geita pamoja na wafanyakazi wote kwa maandalizi na ushiriki wa maadhimisho haya yaliyofanyika kimkoa katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita
Kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kitaifa yamefanyika mkoani Singida katika viwanja vya Bombadia na kauli mbiu ya mwaka huu inasema;
"Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali na kuthamini haki na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki"
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa