Watumishi Waaswa Kuchapa Kazi Kwa Bidii
Watumishi wote wa Umma katika Wilaya ya Geita wameaswa kufanya kazi kwa bidi katika kuwahudumia wananchi kulingana na kada walizoajiriwa nazo ndani ya Utumishi wa Umma.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 13/9/2023 na Mheshimiwa George B. Simbachawene Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipokuwa akizungumza na watumishi wa Umma Wilayani Geita katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita eneo la Magogo.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa kumekuwa na desturi ya baadhi ya watumishi wa Umma kufanya makazi kwa mazoea pasipo kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma na kusahau kuwa wana wajibu wa kuwahudumia wananchi pasipo kuangalia hadhi wala cheo cha mtu.
Waziri Simbachawene ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali watumishi wa umma kwa kuwapandisha vyeo, kulipa malimbikizo ya mishahara na maslahi mbalimbali ya watumishi katika nafasi zao.
Mhe. Simbachawene amewakumbusha Maafisa Utumishi na raslimali watu kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa na kuhakikisha wanatenda haki katika kushughulikia changamoto zinazowakabili watumishi ikiwa ni pamoja na maslahi, upandishwaji vyeo na stahiki mbalimbali.
Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Geita kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Umma mkoani humo na kusikikiliza changamoto za kiutumishi zinazowakabili ili kuzitatua.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa