Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita wametakiwa kushiriki katika michezo mara kwa mara ili kujenga na kuimarisha afya zao. Hayo yamesemwa na Bi. Ellah Makese, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita wakati wa bonanza la michezo lililofanyika leo siku ya Jumamosi tarehe 19 Julai, 2025 katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana Nyankumbu ambapo limeshirikisha watumishi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Bi. Ellah amesisitiza ni vyema Watumishi wakashiriki michezo ili kuimarisha afya, ikiwa watumishi kuendelea kujitokeza katika mabonaza yanayoandaliwa na Mkurugenzi wa Manispaa kupitia Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
Wakati huo Bi. Ellah amekipongeza Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa kwa namna wanavyo andaa na kuratibu mabonanza na ameahidi kuendelea kutoa hamasa kwa watumishi kushiriki akiwa kama Mkuu wa idara ya utumishi na utawala.
Naye, Bi. Ngianasia Kisamo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa, amewapongeza watumishi walivyo jitokeza na kushiriki katika bonaza hili amesema michezo mbali na kujenga afya inaleta upendo na urafiki pia amewashukuru watumishi wa Manispaa ya Kahama kwa kuja kushiriki katika bonaza hili
Katika bonaza hili Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeibuka mshindi wa jumla kwa kushinda michezo 16 kati ya michezo 28 kwa wanaume na wanawake uku ikitoka sare kwa mchezo mmoja. Wakati Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ikishinda michezo 11 na kutoa sare ya mchezo mmoja.
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa