Wananchi wa Nyantorotoro Manispaa ya Geita wamejitokeza kushiriki zaoezi la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Geita huku Mkuu wa wilaya Hashim Komba, kundi la waendesha Pikipiki pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia wakiongoza zoezi hilo
Shughuli hii ya Usafi ni muendezo wa kampeni Ya HYAGULAGA GEITA (SAFISHA GEITA) iliyo zinduliwa na Mhe Mkuu wa wilaya ya geita Hashim Komba Tarehe 26 Aprili, 2025 ikiamasisha watu kufanya usafi na kuisafisha Geita
Nao wanakikundi cha Boda boda wamesema kuwa wataendelea kushilikiana na Mkuu wa Wilaya na viongozi wote kuisafisha Geita
Huku wanawake na Samia wanaunga mkono na kumpongeza Mkuu wa Wilaya kwa kampeni hii inayohimiza usafi hakika amezindua vitu vingi ambavyo wanageita tunatakiwa kutoviacha vipite
Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba anawashukuru wote kwa kujitokeze kuendelea na zoezi la usafi
"Nawashukuru kwa kujitokeza kwa wingi na nawaahidi kuhakikisha na kushirikiana nanyi katika kila hatua ili kuuweka mji wetu uwe safi hii itatuepusha na magonjwa ya mlipuko pia tutachukua hatua za kisheria kuwawajibisha wote wanao puuzia zoezi hili" amesema Mhe. Komba
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa