Akifungua Warsha hiyo katika Ukumbi wa EPZ Bombambili, Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Ndugu Yefred Myenzi amesema, kutokana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, zipo athari mbalimbali. Na lengo la Warshi hii ni kupata data zilizokusanywa ili kudhibiti athari za mazingira, na mradi huu wa kudhibiti taka ngumu kwa kuendeleza miundombinu katika Manispaa yetu ya Geita ambayo ni sehemu ya Mradi wa Bank ya Dunia.
Wadau Mbalimbali wanaoshiriki kutoka Manispaa ya Geita ni walengwa wa mradi GEUWASA, Bonde la Ziwa Victoria, TARURA, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Wote wameaswa kujitoa kikamilifu kusikiliza wasilisho la Mkandarasi kwa lengo Kukagua na kuhakiki takwimu za taka ngumu na usafi wa mazingira zilizokusanywa na Shirika la Open Map Development Tanzania.
Akisisitiza zaidi Mr Patrick Matandala kutoka Banki ya Dunia amesema kuwa takwimu hizi zilizoletwa baada ya upembuzi yakinifu na GAP FUND ni muhimu sana hivyo zichakatwe kwa undani zaidi ili kupata mradi wenye Vigezo sahihi na mji safi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa