• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

Wananchi watakiwa kuendana na kasi ya Awamu ya Tano

Posted on: May 9th, 2018

Wananchi Geita Mji Watakiwa kwenda na kasi ya Awamu ya Tano

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewataka wananchi wote na watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuanzia ngazi ya kijiji kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano kwa kujitolea kikamilifu katika kushiriki kwenye ujenzi wa majengo ya zahanati, vituo vya afya, madarasa na nyumba za walimu ili kujiletea maendeleo katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ametoa agizo hilo tarehe 8/5/2018 wakati wa ziara yake katika vijiji na mitaa ya Halmashauri ya Mji Geita, ambapo alizindua rasmi ujenzi wa zahanati katika Kitongoji cha nyaseke,kijiji cha Igwata, kijiji cha Gamashi katika kata ya Bulela na zahanati ya Mtaa wa Nyakahongola inayojengwa katika kata ya Kasamwa, Halmashauri ya Mji wa Geita.

Mhandisi Robert Gabriel ameagiza vijiji vyote vilivyoko katika Halmashauri ya Mji na Mkoa mzima wa Geita vyenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili  ya ujenzi wa zahanati wahakikishe ujenzi huo unaanza mapema ndani yam waka huu wa fedha. Pia amewasihi wananchi wote kufanya kazi katika sehemu ambayo Mungu amemjalia kila mmoja.

“Naagiza ujenzi wa zahanati zinazojengwa uende sambamba na ujenzi wa nyumba pacha ya watumishi wa zahanati hizo akiwemo mganga, ujenzi huu utakapokamilika mapema utawapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanawake na watoto ambao huwalazimu kutembea zaidi ya kilometa tano kutoka katika maeneo wanayoishi mpaka zahanati za vijiji vya jirani ili kupata huduma za matibabu.” Aliongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi lengo la ziara yake kuwa ni kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kufanya kazi kwa pamoja na kutatua kero na changamoto zinazowakabili. Pia alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha mafundi watakaojenga miundo mbinu hiyo wawe ni wa kujitolea kutoka katika vijiji na mitaa husika na si kuajiri wakandarasi kutoka mikoa ya jirani ili kupunguza gharama za ujenzi na kudumisha uzalendo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bulela Mheshimiwa Salome Kitula amewataka wananchi wake kutotegea katika kazi ya ujenzi wa zahanati na kuwaagiza watendaji wa vijiji kuwalipisha faini watu wote watakaotega katika shughuli hiyo. Kadhalika, Diwani wa Kata ya Kasamwa Mheshimiwa Mary Kasanda amesema kuwa wanakumbana na changamoto ya baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa wa Geita amezindua ujenzi huu ikiwa ni awamu ya tatu ya ziara za aina hiyo katika Halmashauri ya Mji wa Geita, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Apolinary amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zake za kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa Mkoa wa Geita na Halmashauri ya Mji itachangia mifuko 100 kwa kila zahanati iliyoanza kujengwa. Pia amewasihi wananchi wa vitongoji vyote na vijiji vilivyoko katika maeneo yaliyozindua ujenzi kujitolea katika shughuli zote za ujenzi wa zahanati zao.



Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA MAOHOJIANO (ORAL INTERVIEW) KADA YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II September 29, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 05, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KATIKA USAHILI September 21, 2024
  • Zaidi

Habari Mpya

  • BURIANI MHE DAVID CLEOPA MSUYA

    May 07, 2025
  • TWCC MKOA WA GEITA WAMEMKABIDHI HATI YA SHUKRANI MKURUGENZI MYENZI

    May 07, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA GEITA MHE. HASHIM A KOMBA KUTEMBELEA NJIA NA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    May 06, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAMPONGEZA MKURUGENZI MYENZI

    May 05, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • TUWE MFANO KWA TAIFA' Yefred Myenzi
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa