Wananchi Waaswa Kutunza Barabara za Mitaa
Wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Geita wamekumbushwa kuzingatia wanazitunza vyema barabara zinazotengenezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022 Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma hivi karibuni alipokuwa akizindua barabara ya Polisi hadi Rugembe yenye urefu wa kilomita moja ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami nyepesi na Mkandarasi M/S Evax Construction Limited ya mkoani Kagera chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Mijini na vijijini( TARURA).
Ndugu Geraruma amesema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kumeleta manufaa mbalimbali ikiwemo kurahisisha usafiri wa watu na mali zao, kuchochea maendeleo ya wakazi wa maeneo husika kwani baadhi ya watu wamefungua biashara mbalimbali pembezoni mwa barabara na kufanya mandhari ya maeneo husika kuwa ya kuvutia. Hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha hawaruhusu magari yanayozidi uzito kulingana na uwezo wa barabara hiyo kupita hapo.
Pamoja na uzinduzi wa barabara hiyo iliyogharimu Zaidi ya shilingi milioni 449 za kitanzania , Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita umezindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi sita yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.1 na miradi yote kupita bila kipingamizi pamoja na miradi mitano yenye ujumbe mbalimbali ya kupinga rushwa, lishe bora, kutokomeza ugonjwa wa malaria, kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa ya mlipuko na kupinga matumizi ya dawa za kulevya ambapo Kauli mbiu ya mwaka 2022 ni “ Sensa ni msingi wa Mipango ya maendeleo: Shiriki kuhesabiwa, tuyafikie maendeleo ya Taifa.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa