Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Geita kuwa sehemu ya mfano kwa kuzingatia usafi katika mazingira yanayowazunguka kwa hiari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa (aliyesimama juu ya kiti),akizungumza wakati akizindua Kampeni ya usafi wa mazingira uliofanyika leo Januari 29,2022 Mkoani Geita.
Waziri Bashungwa ametoa wito huo leo Januari 29, 2022 wakati akizindua wa Kampeni ya usafi wa mazingira Mkoa wa Geita na kauli mbiu ya “Usafi wa Geita ni wajibu wangu, Mazingira bora ni ni fahari yangu”
“Utaratibu mliouweka kila wiki kufanya usafi mshirikiane na makapuni yanayochimba dhahabu hapa Geita na wadau wengine kuhakikisha tunakuwa na Geita safi inayomelemeta” amesema Bashungwa
Aidha, Waziri Bashungwa amewataka wasafiri wote kubadilika kwani kuna baadhi ya watu wanapanda daladala na mabasi ya kwenda mikoa wakimaliza kunywa soda na biskuti au kitu chochote kilicho kwenye mfuko au chupa wakimaliza kutumia wanatupa dirishani kitu ambacho ni uvunjifu wa sheria ya mazingira na sheria za usalama barabarani hivyo tunapaswa kubadiika ili kuweka mazingira safi.
Pia, Waziri Bashungwa amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Geita Mjini kushirikiana na na Baraza la madiwani kuweka mikakati ya kuboresha stendi ya mkoa ili kuwa na stendi bora na ya kisasa inayotambulisha Mkoa wa Geita.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule ameeleza kuwa wamekubaliana na wananchi kuhakikisha kila mtu anatunza mazingira katika eneo lake ambapo zoezi la kufanya usafi litakuwa endelevu na litafanyika kila Jumamosi ya kila wiki na kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi zoezi hili litafanyika kwa pamoja kama leo hii.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi wa mazingira uliofanyika leo Januari 29,2022 Mkoani Geita.
Uzinduzi wa Kampeni hiyo ya usafi ni utekelezaji wa Maelekezo ya Waziri Bashungwa aliyoyatoa kwa Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya zote nchini kuhakikisha wanasimamia suala zima la usafi hususani katika miradi yote ya barabara, masoko na stendi.
Katika uzinduzi huu Taasisi mbalimbali za kiserikali, binafsi na za dini pamoja na wananchi zimeungana katika kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa zikiwemo vyombo vya Ulinzi na usalama, Mamlaka ya mapato Tanzania, Shirikia la Umeme, RUWASA, TARURA, GGML, GEUWASA, CRDB Bank, NMB Bank, NBC Bank, shirika la Posta Tanzania, Plan International na Madhehebu mbalimbali ya Dini.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa