Wanafunzi wanufaika waishukuru TASAF
Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Kalangalala katika Halmashauri ya Mji Geita wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jam
(TASAF) awamu ya tatu ambao umelenga kunusuru kaya maskini kwa kuziwezesha familia zao kuweza kujikimu kimaisha.
Wanafunzi hao wametoa shukran i hizo walipotembelewa shuleni kwao na Maafisa kutoka TASAF hivi karibuni.
“Najisikia vibaya kuchelewa kuanza shule kwa sababu baba yangu alikosa fedha ya kuninunulia sare za shule, laiti mzazi wangu angekuwa na uwezo ningekuwa kidato cha kwanza mwaka huu”. Ni kauli ya hisia aliyoisema mwanafunzi Mishangi Jonas mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo. Mishangi amesema baada ya TASAF kuiwezesha familia yake, baba yake ameweza kumnunulia sare mpya, kupata chakula kwa milo mitatu na kiwango chake cha ufaulu kimepanda kutoka nafasi ya 12 kati ya 217 darasani hadi nafasi ya kwanza hivi sasa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkombozi Lembo ambaye ni msimamizi wa wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini amesema kuwa jumla ya wanafunzi 55 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi Kalangalala wanahudumiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii. Mwl. Lembo ameishukuru TASAF kwa mchango wao katika elimu kwani mwenendo wa kitaaluma wa wanafunzi hao awali haukuwa mazuri lakini baada ya mpango wa TASAF maendeleo yao kimasomo yamepanda na wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wanafaulu vizuri kuendelea na masomo ya sekondari.
Mwalimu Lembo ametoa ushauri kwa TASAF kuendelea kutoa elimu kwa wakuu wa kaya
(wazazi au walezi) ili waweze kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuwahudumia watoto wao mahitaji muhimu ya shule na watambue umuhimu wa wao kama wazazi au walezi kusimamia maendeleo yao kitaaluma. Kuna wazazi wanajitahidi kutimiza wajibu wao lakini baadhi yao hutumia fedha wanazopewa kwa manufaa yao binafsi pasipo kuwakumbuka watoto wao ambao ni wanafunzi.
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji Geita Ndg. Upendo Kilonge amesema jumla ya walengwa 4659 kutoka katika vijiji 13 na mitaa 27 ndani ya Halmashauri ya Mji wako katika mpango wa kunusuru kaya zisizojiweza.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa