Walimu Waweka Mikakati ya Kushinda UMITASHUMTA
Walimu wa michezo na Sanaa wa shule zote za msingi katika Halmashauri ya Mji Geita wameketi kujadili mikakati ya namna ya kufanya vizuri katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yatakayoanza kuanzia mwezi Machi 2024.
Kikao kazi hicho kilichowajumuisha walimu wa Sanaa na michezo pamoja na maafisa wa Idara ya elimu na kitengo cha Sanaa, utamaduni na michezo kimefanyika tarehe 21/02/2024 katika ukumbi wa Ofisi kuu ya Halmashauri ya Mji Geita kikiwa na Agenda ya kupitia mwongozo wa uendeshaji wa michezo na Sanaa shuleni pamoja na mashindano ya UMITASHUMTA.
Mkuu wa Idara ya Elimu msingi Bi. Margareth Macha amewaasa walimu hao kuepukana na desturi ya kuwaingiza kwenye mashindano wanafunzi wenye umri mkubwa tofauti na walioainishwa kwenye mwongozo wa mashindano na kushirikiana na Halmashauri katika kutafuta wadau mbalimbali watakaochangia mahitaji kama vile vifaa vya michezo, sare, chakula kambini katika ngazi ya shule, kata na tarafa.
Mikakati iliyowekwa ili kufikia malengo ni pamoja na kuandaa timu za wanafunzi katika michezo yote mapema, kufanya maandalizi ya viwanja vya michezo hata kama ni vidogo, walimu wa michezo waonyeshe dhamira ya dhati kuwasaidia Watoto kukuza vipaji vyao.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake Afisa Elimu Kata ya Nyanguku Bi. Kuwepo na utaratibu mzuri wa upokeaji wa risiti za michango ya UMITASHUMTA, Walimu wakuu watoe ushirikiano na kuwathamini walimu wa Sanaa na michezo katika shule zao.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa