• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Geita Town Council
Geita Town Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Rasilimali Watu na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Miundombinu, Maendeleo vijijini na Mjini
      • Usimamizi taka na Usafi wa Mazingira
    • Vitengo
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Sheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uchimbaji Madini
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya, Ustawi wa jamii na Huduma ya Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Elimu na Afya
      • Kamati ya Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu ya Maombi
    • Miongozo
    • Jarida la Halmashauri
    • Mkakati wa kuziwezesha
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
  • Maeneo ya Uwekezaji

Wakurugenzi Waagizwa Kutenga Bajeti za Madampo

Posted on: June 7th, 2022

Wakurugenzi Waagizwa kutenga Bajeti za Madampo

Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Geita wameagizwa kuandaa bajeti za ujenzi wa madampo ya kisasa ili usafi unapofanyika taka ziweze kuhifadhiwa na kuchakatwa bila kuchafua mazingira.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu katibu Tawala mkoa wa Geita Ndg. Herman Matemu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Geita  akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani mwaka 2022 yaliyofanyika  kimkoa katika viwanja vya shule ya sekondari ya Wasichana Nyankumbu Geita mjini hivi karibuni.

Ndg. Matemu  amesema kuwa Halmashauri zinapoandaa bajeti zao wahakikishe kwamba zinakuwa na bajeti hiyo  ili madampo ya kisasa yaweze kujengwa katika kila Halmashauri. Pia amesema ni wajibu wa kila mwananchi kuanzia ngazi ya familia kujitafakari ni kwa kiasi  gani maamuzi anayoyafanya yanaweza kutunza mazingira na kwa ngazi ya taasisi ni kwa kiasi gani waajiri na wenye mamlaka wanatambua umuhimu wa mazingira na kuhamasisha upandaji miti.

Katika taarifa ya utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira iliyosomwa na kaimu katibu tawala mkoa Geita Charles Chacha,  imebainika kwamba hali ya mazingira katika machimbo hutofautiana ambapo wachimbaji wakubwa na wakati ni salama kwa shughuli za hifadhi za mazingira huku  wachimbaji wadogo ndiyo wenye changamoto katika uhifadhi wa mazingira.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba mkoa wa Geita una misitu hekta laki mbili mia tano hamsini na nane nukta tatu (200,558.3) kati ya maeneo hayo sita yanamilikiwa na wakala wa misitu Tanzania- TFS, maeneo mengine sita yanamilikiwa na mamlaka za Serikali za mitaa.

“Pamoja na kuwa na misitu ya asili mkoa wa Geita umepanda miti milioni tatu, mia nane ishirini na tano ,mia tatu kumi na tatu kwa mwaka wa  2021/2022” alisoma Charles chacha.

Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kwamba Malengo ya upandaji miti ilikuwa ni kufikia milioni tisa lakini, miti iliyopandwa ni milioni tatu, mia nane ishirini na tano ,mia tatu kumi na tatu na miti iliyopona ni milioni tatu themanini elfu  mia saba hamsini na tatu huku miti hiyo iliyopandwa ni  sawa na asilimia 42.5% .

Charles Chacha amesema changamoto kubwa iliyokwamisha kufikia malengo ni upungufu wa miche ya miti, hivyo serikali imeweka mikakati ya kuyafikia malengo hayo kwa kutumia taasisi zake 66 za elimu na mpaka sasa miche  milioni mbili imeshapatikana.



Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA MAOHOJIANO (ORAL INTERVIEW) KADA YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II September 27, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II September 29, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 05, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KATIKA USAHILI September 21, 2024
  • Zaidi

Habari Mpya

  • BURIANI MHE DAVID CLEOPA MSUYA

    May 07, 2025
  • TWCC MKOA WA GEITA WAMEMKABIDHI HATI YA SHUKRANI MKURUGENZI MYENZI

    May 07, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA GEITA MHE. HASHIM A KOMBA KUTEMBELEA NJIA NA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    May 06, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAMPONGEZA MKURUGENZI MYENZI

    May 05, 2025
  • Zaidi

Video

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA ITIKADI ZA KISIASA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Mfumo wa Watumishi kujihudumia
  • Applications Forms
  • Acts
  • Taarifa za Huduma za Afya
  • Mfumo wa Kupata Leseni za Biashara ( Mfumo wa Tausi)
  • Barua pepe za watumishi
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Taarifa za Mapato

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • TUWE MFANO KWA TAIFA' Yefred Myenzi
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Geita Tanzania

    Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita

    Namba ya Simu: 0282520437

    Mobile:

    Barua pepe: td@geitatc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

Visitors Counter

Counter Widgets

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa