Viongozi Wa Serikali Za Mitaa Waagizwa Kuwa Waadilifu
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni wameaswa kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya viongozi wa Serikali.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuapishwa viongozi 436 kutoka katika Tarafa ya Geita yenye kata nane, kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Josephat Maganga licha ya kuwapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa na wananchi amewataka viongozi hao kujiamini kama viongozi katika ngazi ya mitaa.
Mhe. Josephat Maganga amesema kuwa wananchi watakaosimamiwa wana haki zao hivyo viongozi wana jukumu la kusimamia haki hizo kwa kusikiliza shida mbalimbali zinazowakabili pasipo na ubaguzi na kuwatatulia kero zinazowakabili.
“Mmepata nafasi ya kuwaongoza wananchi, hivyo viongozi mnatakiwa muwaelekeze vizuri pia kama viongozi ni lazima mshiriki katika kupanga mipango ya mitaa na vijiji katika kuibua na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.”
Afisa Tarafa wa Geita Mjini Ndg. Innocent Mabiki amewashauri viongozi hao kuhakikisha wanatetea haki za wananchi na sio kujifanya wakuu, ogopeni kuwa vikwazo kwa wananchi mnaokwenda kuwaongoza.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake Bw. Sosthenes Calist ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa Msalala Road ameahidi kuwatumikia wananchi kwa moyo na ameomba ushirikiano kutoka kwa wananchi wake ili waweze kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoko katika eneo lake na kujipatia maendeleo binafsi na ya Taifa kwa ujumla.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa