Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Ndugu Yefred Mayenzi, ametoa elimu kuhusu mbinu za kuzuia uchepushwaji na utoroshwaji wa mapato yatokanayo na ushuru wa madini kwa wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea pamoja na viongozi kutoka serikali ya Kata ya Nditi na Kijiji cha Nditi. Mafunzo hayo yalitolewa, Juni 25, 2025, katika Manispaa ya Geita.
Elimu hiyo ni sehemu ya malengo ya ziara ya mafunzo iliyoratibiwa na Halmashauri ya Nachingwea, ambapo wataalamu na viongozi wa kijiji walitembelea Geita kwa lengo la kujifunza namna bora ya uendeshaji wa migodi, usimamizi wa rasilimali za madini, na uimarishaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato.
Kata ya Nditi inatajwa kuwa na mgodi wa madini mbalimbali kama Nickel, Copper, na mengineyo. Hata hivyo mapema tarehe 26 juni 2025 viongozi hao wamepata nafasi ya kutembelea Kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mining Limited (GGM) nakupata elimu namna bora ya uendeshaji wa shughuli za migodi kwa kuzingatia sheria, usalama, na maendeleo ya jamii, ili waweze kusimamia vyema rasilimali hizo kwa manufaa ya wananchi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
TUFUATILIE KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII
Instagram
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa