Geita Mji Yazindua uogeshaji Mifugo
Halmashauri ya Mji wa Geita imezindua rasmi zoezi la uogeshaji wa mifugo ambapo ng’ombe 27,634, mbuzi 25,148 na kondoo 8,907 wanataraji kuogeshwa katika zoezi hilo. Uzinduzi huo ulifanyika katika kata ya Bulela hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Afisa Tarafa wa Geita Ndg. Innocent Mabiki aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Geita alisema lengo la zoezi hilo ni kutokomeza magonjwa ya kupe na mbun’go ambapo asilimia 68% ya vifo vya mifugo vinasababishwa na magonjwa hayo.
Ndg Mabiki aliongeza kuwa kuogesha mifugo kutaondoa hasara za kuharibika kwa ngozi za mifugo,kupungua kwa uzalishaji wa maziwa na nyama pamoja na kuongezeka kwa udumavu unaoleteleza mnyama kuchelewa kufikia uzito wa kuuzwa na kuzaa. Pia mfugaji yoyote atakayekaidi zoezi hili atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufungwa kifungo cha miezi sita au faini ya laki tano.
Daktari wa mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Geita Jasson Mutayabarwa amesema kuwa serikali itaendelea kutoa dawa ya kuogesha aina ya paranex kila baada ya miezi sita, pia mfugaji atatakiwa kuchangia shilingi 600 kwa kila ng’ombe, shilingi 150 kwa kila mbuzi na kondoo kwa ajili ya kuongeza dawa pale inapopungua wakati wa kuogesha.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoia imeamua kufufua majosho kwa kutoa dawa aina ya paranex nchini ili iwe chachu kwa wafugaji kuanza kuogesha mifugo yao kwa kutumia majosho dhidi ya magonjwa yaenezwayo na kupe pamoja na mbun’go.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa