Ushirikiano ni Nyenzo Muhimu Katika Utumishi- Bandisa
Watumishi wa Umma katika Halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita wameaswa kushirikiana kikamilifu kwa kufanya kazi kwa uwazi, usawa na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao kwenye ofisi zao ili kuwa na matokeo chanya.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Ndugu Denis Bandisa Tarehe 21/06/2019 katika Ukumbi wa Gedeco, Halmashauri ya Mji Geita alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri mbili zilizoko katika Wilaya ya Geita kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
“Taasisi haiwezi kujengeka kama Wakuu wa Idara na Vitengo hamshirikiani, hamgawani raslimali zilizopo ,hakuna uwazi kati yenu na watumishi walioko chini yenu. Acheni tabia ya kujilimbikizia majukumu na kuwa wabinafsi, siri ya mafanikio ya Taasisi yoyote zikiwemo Halmashauri zenu ni kugawana raslimali chache zilizopo.” Aliongeza Ndg. Bandisa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi kutekeleza majukumu yao kulingana na mpango kazi aliojiwekea. Pia watumishi wa Umma wanatakiwa kujiandaa kwa masuala mahsusi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wapiga kura kwa kuwaelimisha wananchi katika maeneo yao.
Ndugu Denis Bandisa ametembelea Halmashauri zote katika Mkoa wa Geita ikiwa ni programu iliyoandaliwa na Mkoa katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Tarehe 16-23/6/2019 kwa kukutana na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa wa Geita
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa