USALAMA ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii katika ngazi zote, na kwa hakika hakuna jamii ambayo itajivunia kupata mwelekeo wa maendeleo Kama kwao usalama haupo.
"Ulinzi na Usalama ndiyo msingi wa mambo yote" amesema DC Komba
Mhe. Komba ameyasema hayo mara baada ya ukaguzi wa nyumba ya Polisi katika Kata ya Mgusu. Mhe. Komba amewataka Wananchi na jamii kwa ujumla kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo wakati ikiwemo kutoa taarifa za uvunjifu wa amani katika mamlaka husika na ikiwezekana kutoa taarifa moja kwa moja kwake.
Aidha, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mgusu Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wawekezaji wote kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka.
Kabla ya mkutano huo wa hadhara Mhe. Komba alianza na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya sekta afya, elimu na Barabara.
Katika ziara hiyo, Mhe. Komba aliambatana na Katibu Tawala Wilaya, Kamati ya Usalama Wilaya, Kaimu Mkurugenzi wa Mji, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Mji, Afisa Tarafa ya Geita na Wakuu wa Taasisi za TANESCO, TARURA na GEUWASA
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa