Hayo yamesemwa leo tarehe 29 Julai, 2024 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita ambaye ndiye Afisa Muandikishaji wa Jimbo la Geita Mjini Ndg. Yefred Myenzi wakati akifungua mafunzo kwa Watendaji wa uboreshaji wa dafatri la kudumu la wapiga kura ngazi ya jimbo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Geita
"Lazima tuwe wasikivu, tuwe makini, tuzingatie yale ambayo tunaelekezwa na wataalam wetu wa tume huru ya mafunzo na wengine ambao watawapatia mafunzo, umakini wetu utarahisisha hii kazi angalau kwanza tufanye kwa muda mfupi lakini pia kuikamilisha kwa ufanisi unaotarajiwa na viwango vinavyotarajiwa" amesema Ndg. Myenzi
Mafunzo haya ya ngazi ya Jimbo yanatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 30 Julai, 2024 ambapo yatafuatiwa na mafunzo ngazi ya Kata kwa watendaji wa vituoni (Waandishi wasaidizi na Waendashaji wa vifaa vya bayometriki) yanayotarajiwa kufanyika tarehe 2 hadi 3 Agosti, 2024 kwa mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha kwa Jimbo hili la Geita Mjini zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya kwanza unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 05 hadi 11 Agosti, 2024. na wito unatolewa kwa wananchi wote wenye sifa na wapiga kura wa Jimbo la Geita kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Watendaji wa Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakifuatilia mafunzo
Afisa Muandikishaji Ngazi ya Jimbo Bi. Lucy Lyaruu akisisitiza jambo wakati wa mafunzo
Naye, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari ametembelea mafunzo hayo ya watendaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmashauri ya Mji Geita ambapo amewaasa watendaji hao kufanya kazi Kwa weledi na kutoa huduma nzuri kwa wananchi watakaojitokeza kujiandikisha na wapiga kura watakaokwenda vituoni kuboresha taarifa zao.
Mhe. Asina Omari akizungumza jambo katika mafunzo
Uboreshaji huu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaenda sambamba na kauli mbiu inayosema;
"Kujiandisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa