Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Ndugu Yefred Myenzi leo Tarehe 8 Januari 2025 katika Ukumbi wa Gedeco amefanya kikao na watumishi wote wa Makao makuu Watendaji wa Kata, Mitaa, Vijiji na Waganga wafawidhi kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya utendaji kazi hasa katika kipindi hiki ambapo Halmashauri imepanda hadhi na kuwa Manispaa . Pia amepokea taarifa ya tathmini ya utendaji kazi kwa kipindi cha Mwezi Julai - Desemba 2024. Akiwa katika kikao hicho ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa GEDECO uliopo Manispaa ya Geita ameeleza kuwa kitendo cha Halmashauri kupanda hadhi nakuwa Manispaa ni heshima kubwa kwani inaifanya Halmashauri kuwa na mipango mikubwa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na upangaji mzuri wa maeneo ya Makazi Biashara na Burudani.
pamoja na hayo amehimiza watumishi kwenye idara zinazojihusisha na burudani kuwa na ubunifu mkubwa wa matamasha mbalimbali yatakayo ifanya manispaa kupata mapato na kuchangamka muda wote.
Pia katika kikao hicho Mkurugenzi amesisitiza mambo matano muhimu ambayo ni Majukumu ya Msingi ya Halmashauri
1.Kukusanya Mapato.
2.Kuhakikisha Mapato yanatumika kuleta Maendeleo.
3.Kutoa Huduma Mbalimbali kama Afya, Elimu
4.Kutatua Kero Mbalimbali zilizoko katika Jamii.
5.kuhakikisha Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi Myenzi amesisitiza kila mmoja kuzingatia suala la Ukusanyaji wa Mapato na kuwakumbusha kuwa mapato hayo yanayokusanywa hutumika kujenga na kutatua changamoto mbalimbali katika Manispaa ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Ofisi, Hospitali, Shule n.k. Pamoja na mambo mengine amewakumbusha watumishi kuendelea kuwa na umoja wanapokuwa kazini na katika jamii amewaeleza kuwa Halmashauri inayo majukumu mengi makubwa kupitia idara zake hivyo ameendelea kuwaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii kila wanapopewa Jukumu. Katika Kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa Utumishi Bora, Afisa utumishi Halmashauri ya Mji Geita Ndugu Mussa Mbyana amewaeleza na kuwasomea kanuni taratibu na miongozo ya kitumishi ikiwa ni pamoja na kuzingatia mavazi yenye muonekano mzuri usio tia shaka. pia amewashauri watumishi kuzingatia vitu wanavyokwenda kusomea hasa wanapohitaji kwenda kuongeza elimu zao amesema kuwa sio kila kitu kinachofundishwa kinafaa kutumika katika shughuli za kiofisi hivyo wanapaswa kuangalia kwa umakini fani wanazokwenda kusomea na faida zake ili kuepuka kupoteza muda .Amewataka pia watumishi kujiandaa vyema hasa wanapoelekea katika kipindi cha kustaafu kwani kumekuwa na changamoto nyingi hususan watumishi wanapostaafu bila kujiandaa.
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa