Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba amewataka Viongozi wa ngazi za Wilaya hadi Mtaa na Vijiji kwenda kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kuacha tabia ya kukaa maofisini.
Mhe. Komba ameyasema hayo alipokuwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Soko la Mtaa wa Nyakato lililopo Mtaa wa Nyakato katika Kata ya Nyanguku. Mhe. Komba ameanza ziara yake ya kutembelea Kata zote za Halmashauri ya Mji Geita lengo kuu likiwa kujitambulisha, kuijua Halmashauri ya Mji wa Geita, Kutembelea na kukagua miradi iliyokwama ili iweze kukamilishwa na kuanza kutoa huduma lakini pia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majibu.
Wananchi wa Kata ya Nyanguku wakifuatilia mkutano
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia wananchi kwa kuwafuata katika maeneo yao kusikiliza kero zao na kuzitafutia majibu.
Mhe. Rais Samia alitoa maagizo hayo Septemba 17, 2023 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Boma uliopo Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara.
Mhe. Komba ameeleza kusikitishwa kuona kero za Wananchi wa Vijijini na Mtaa zinafika mpaka Wilayani wakati kwenye maeneo yao kuna Viongozi wa ngazi zote ambao wanaweza kuzitatu kero hizo.
Wakati huo huo Mhe. Komba amewataka watendaji wote wa Kata, Mitaa na Vijiji kuhakikisha wanakuwa na Madawati ya kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi na kuzitafutia majibu na kero ambazo hazitapatiwa majibu ndiyo zipande ngazi ya juu.
Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Komba ametembelea miradi mbalimbali muhimu ikiwemo ya afya, elimu, maji, barabara na kusikiliza kero zao na kuzitafutia majibu.
Mhe. Komba (Mwenye Kaunda Suti) akiwa katika ukaguzi wa mojawapo ya Mradi
Katika ziara hiyo, Mhe. Komba alifuatana na Katibu Tawala Wilaya, Kamati ya Usalama Wilaya, Mkurugenzi wa Mji, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Mji, Afisa Tarafa ya Geita na Wakuu wa Taasisi za TANESCO, TARURA na GEUWASA
Geita Tanzania
Sanduku la Posta: P.o Box 384 Geita
Namba ya Simu: 0282520437
Mobile:
Barua pepe: td@geitatc.go.tz
Hatimiliki 2017 Halmashauri ya Mji Geita . Haki zote zimehifadhiwa